Papa ajaye atakabiliana na hoja ngumu
7 Mei 2025
Matangazo
Katika misa ya mwisho kabla ya kufunguliwa kwa kongamano la kupiga kura, Kadinali Giovanni Battista Re pia alitoa wito kwa makadinali hao watakaopiga kura kudumisha umoja wa Kanisa, akisema ni uamuzi wa muhimu wa kipekee, na kila fikira za kibinafsi lazima ziwekwe kando.
Soma pia: Merkel: Ni vyema Papa ajaye akafuata mkondo wa Papa Francis
Waumini wa Kanisa Katoliki na wafuatiliaji wengine kote duniani watasubiri ishara ya kuchaguliwa kwa papa mpya kupitia moshi utakaotoka kwenye chimni iliyofungwa juu ya Kanisa la Sistine.
Moshi mweupe utakapofuka itakuwa ni ishara kuwa baraza hilo la makadinali limefanikiwa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa Katoliki.