1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa akutana na wahamiaji nchini Hungary

29 Aprili 2023

Papa Francis leo hii aingia siku yake ya pili kati ya ziara yake ya siku tatu nchini Hungary ambapo amekutana na makundi maalum ya watu.

Ungarn I Papst Franziskus besucht Budapest
Picha: Marton Monus/REUTERS

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, akiwa katika siku yake ya pili, kwenye ziara yake ya siku tatu nchini Hungary leo hii amekutana na watu maskini na wakimbizi mjini Budapest.Katika mkutano wake katika kanisa la Mtakatifu Elizabeth, kiongozi huyo mkuu wa kanisa amerejea wito wake wa takwa la kujitolea kuisadia jamii ya watu wenye uhitaji wa huduma muhimu.Sera ya wakimbizi ya serikali ya Hungary ina utata barani Ulaya. Sheria za taifa hilo mara nyingi zinakinzana na sheria za kimataifa na za Umoja wa Ulaya. Kanuni zake haziruhusu kwa watu ambao wameingia katika mipaka ya taifa hilo eneo la kuomba hifadhi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW