1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Papa asikitishwa na vifo vya wafanyakazi wa misaada Gaza

3 Aprili 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya wafanyakazi saba wa mashirika ya kutoa misaada waliouwawa na mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Kanisa Katoliki |Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis Picha: Yara Nardi/REUTERS

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya wafanyakazi saba wa mashirika ya kutoa misaadawaliouwawa na mashambulizi ya Israel, walipokuwa katika harakati za kuwasilisha misaada huko Gaza.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kila wiki Baba Matakatifu mwenye umri wa miaka 87 amesema, anaziombea familia za wafanyakazi hao na kutoa wito wa njia za uwasilishwaji misaada kwa watu wa Gaza kufunguliwa na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.Marekani, Uingereza na EU zalaani mauaji kwa watoa misaada

Wito huu wa Papa Francis unakuja wakati ambapo Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amesema leo kuwa, shambulizi hilo la Israel limevuruga mahusiano ya nchi hizo mbili na kwamba Israel inauweka uungaji mkono wa Poland kwake katika mtihani mkubwa.

Haya yanafanyika wakati ambapo wizara ya afya ya gaza inayoendeshwa na kundi la Hamas, imesema kufikia sasa Wapalestina karibu 33,000 wameuwawa kutokana na mashambulizi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW