1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa atoa wito wa kuwepo amani duniani

21 Agosti 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki dunini, Papa Francis amerudia kutoa wito wa kuwepo amani, wakati ambapo maeneo kadhaa ulimwenguni yanakabiliwa na vita.

Papa Francis 2015
Papa Francis akiwabariki watoto alipotembelea kambi ya wakimbizi, mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Novemba 29, 2015.Picha: L'Osservatore Romano/AP Photo/picture alliance

Akizungumza na waumini katika utaratibu wake wa kawaida kila Jumatano, Papa Francis amewataka Wakristo kuwakumbuka wote wanaoteseka katika nchi zote zenye vita, pamoja na mashahidi wanaouawa Ukraine, Palestina, Israel, Myanmar, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hata hivyo, Papa Francis amekiri kuwa kwa bahati mbaya wakati mwingine Wakristo hawaenezi upendo wa Yesu Kristo, na kuonya kuwa dhambi huwaondoa Wakristo kwa Yesu na huwaleta karibu na pepo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW