1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa azungumzia juu ya machafuko hotuba yake ya kila mwaka

8 Januari 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ametoa hotuba ya kila mwaka mbele ya wanadiplomasia wanaoyawakilisha mataifa yao kwenye makao makuu ya kanisa mjini Vatican.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa FrancisPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Papa Francis amezungumzia masuala kadhaa ikiwemo vita, uhamiaji, mzozo wa mabadiliko ya tabianchi na uundaji wa silaha za maangamizi.

Kuhusu vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine pamoja na mzozo wa Israel na kundi la Hamas huko Gaza, Papa Francis amesema mashambulizi yasiyobagua kwenye uwanja wa vita ni uhalifu kwa sababu ni kinyume na sheria ya kimataifa.

Soma pia:  Papa ahimiza huruma kwa wanawake na watoto wanaonyanyasika

Kiongozi huyo wa kiroho aligusia kwa kirefu mzozo wa Mashariki ya Kati akirejea msimamo wa kanisa juu ya suluhisho la kuundwa madola mawili kama njia ya kumaliza uhasama kati ya Israel na Palestina.

Papa Francis pia amekosoa wimbi la mapinduzi barani Afrika na chaguzi kwenye baadhi ya nchi za bara hilo alizosema ziligubikwa na "rushwa, vitisho na vurugu."

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW