1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedict wa kumi na sita alaumiwa kwa kutoonyesha huruma kwa maangamizi yaliyofanywa dhidi ya wayahudi.

Jason Nyakundi12 Mei 2009

Papa Benedict alitembea maeneo takatifu kabla ya kuongoza misa iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini katika shamba la Gethsemane mjini Jerusalem.

Papa Benedict akijitayarisha kuingia katika msikiti.Picha: AP

Spika wa Bunge la Israel Reuven Rivlin, amemlaumu baba mtakatifu Benedict wa kumi na sita kwa kutotilia maanani na pia kwa kutoonyesha huruma dhidi ya mateso waliyoyapata Wayahudi na kuongezea zaidi lawama zinazomwaandama Papa Benedict akiwa ziarani katika eneo la mashariki ya kati.

Akiwa nchini Israel, Papa Benedict hii leo aliyatembelea maeneo matakatifu ambapo alifanya maombi katika eneo takatifu la Wayahudi pamoja na maeneo matakatifu ya Waislamu.

Papa mtakatifu, mzaliwa wa ujerumani, alisimama kwa maombi kwa dakika chache kwenye jengo ambalo ni eneo takatifu zaidi baada ya kukutana na kiongozi wa Kiislamu wa Kipalestina.

Papa Benedict aliondika ujumbe katika ukuta wa eneo hilo takatifu kabla ya kukutana na viongozi wakuu wa dini ya Kiyahudi.

Ujumbe huo ulisema: nawatumia amani katika nchi hii takatifu, katika mashariki ya kati na katika familia yote ya wanadamu. Papa pia aliwaomba wakazi wote wa Mashariki ya Kati waishi kwa mani.

Kwa sasa hivi papa Benedict anaongoza misa katika shamba la Gethsemane iliyohudhuria na maelfu ya waumini, waliopeperusha bendera za palestina za vatican pamoja na za Israel.

Akizungumzia kujiunga kwa Papa Benedict katika jeshi la ujurumani wakati wa ujana wake, spika wa bunge la Israel, Reuven Rivlin, alimkemea Papa Benedict kutokana na matamshi yake hapo jana, Jumatatu, kuhusu maangamizi ya Wayahudi milioni sita.

Alikuja akatuhutubia kama mwana historia,akajitenga na yale ambayo hayangehitajika kufanyika, na sasa utafanya nini? Rivlin alikiambia kituo cha radio cha Israel.

Papa Benedict akiwa na viongozi wa Israel katika maeneo takatifu.Picha: AP

Kiongozi wa dini ya kiyahudi Yisrael Meir Lau mjini Jerualem, alisema kuwa, Papa John Paul wa pili ambaye ni mtangulizi wake papa Bebedict wa kumi na sita, alizungumzia maangamizi yaliyotekelezwa dhidi ya mamilioni ya Wayahudi yaliyofanywa na utawala wa Manazi.

Hata kama Papa Benedict alizungumzia maangamizi ya wayahudi, aliwakasirisha viongozi wengi wa Kiyahudi waliosema kuwa angeomba msamaha kama Mjerumani na pia kama Mkiristo kutokana na maangamizi hayo.

Hata hivyo, msemaji wa makao makuu ya Vatikani alimtetea Papa Benedict hii leo na kusema kuwa hakuwa mwanachama wa kundi lililokuwa likiongozwa na Hitler.

Kasisi Federico Lombardi alisema kuwa Papa Benedict, ambaye matamshi yake ya hapo jana yaliwakasirisha Waisrael, alisema kuwa baba mtakatifu alikuwa kwenye kikosi cha ulinzi wa anga ambacho vijana wengi walijiunga nacho miaka miwili ya mwisho wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Kikosi hicho cha walinzi wa anga ambacho papa alijiunga nacho mwisho mwisho wa vita vikuu vya pili vya dunia hakikuwa na uhusiano hata kidogo na kikundi cha Hitler, Lombardi alisema.

Papa Benedict anaitembelea Israel baada ya kukamilisha ziara yake nchini Jordan katika juhudi za kumaliza tofauti kati ya Wayahudi na Waislamu, siku moja baada ya matamshi makali yaliyotolewa na kiongozi mahakama za Kiislamu na kuyaghadhabisha makao makuu ya Vatikani pamoja na Israel.

Sheikh Taiseer al Tamimi, ambaye hakuwa miongoni mwa wazungumzaji, alichukua kipaza sauti baada ya Papa Benedict kumaliza kutoa hotuba yake, na kusema kuwa ni lazima Wakiristo pamoja na Waislamu waungane dhidi ya Israel.

Mwandishi Jason Nyakundi/AFP

Mhariri Othman miraji



Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW