1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis aanza ziara ndefu zaidi ya nje

2 Septemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameanza ziara ya nje hii leo, akitarajiwa kuzuru mataifa manne ya Kusini Mashariki mwa Asia na Oceania.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis akipanda ndege.
Papa ameanza safari yake ndefu zaidi licha ya wasiwasi wa kiafyaPicha: picture alliance / AP Images

Ziara hiyo ya siku 12, ndio ndefu zaidi kufanywa na kiongozi huyo tangu aliposhika wadhifa huo.

Papa Francis ameondoka Rome mapema leo na atazuru Indonesia, taifa lenye idadi kubwa zaidi ya waumini wa Kiislamu wapatao milioni 240. Kisha atakwenda Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore. 

Soma pia: Papa Francis atoa mwito wa msaada zaidi kwa wagonjwa wa mpox

Ziara hiyo ya 45 ya Papa Francis nje ya nchi itajikita hususani kwenye masuala ya amani na ushirikiano baina ya dini tofauti. Ni Timor ya Mashariki tu ambako kuna idadi kubwa ya waumini wa Roman Katoliki.
 
Ziara kubwa ya mwisho ya Papa Francis ilikuwa mwaka mmoja uliopita, alipozuru Mongolia. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW