1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis abadilisha idara za mafundisho ya kiimani

14 Februari 2022

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amebadilisha idara za mafundisho ya kiimani, ambazo zitakuza na kutetea mafundisho ya Kikatoliki

Italien Vatikan Papst hält Neujahresmesse
Picha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amebadilisha idara za mafundisho ya kiimani, ambazo pamoja na kukuza na kutetea mafundisho ya Kikatoliki pia zitakuwa na jukumu la kushughulikia kesi za unyanyasaji ndani ya Kanisa.

Soma pia: Papa Francis awataka waumini wa Kanisa Katoliki wawasaidie masikini

Sehemu ya amri hiyo ya Papa iliyochapishwa leo imesema kufuatia mabadiliko hayo kutakuwa na idara mbili badala ya tatu, ambazo kila moja itakuwa na katibu wake.

Papa Francis aidha ameigawanya mamlaka ya Vatican, upande mmoja ukihusika na mafundisho na upande mwingine utashughulikia nidhamu, na utawala pia umegawanywa kwa kuzingatia idara hizo mbili, badala ya mtu mmoja kama ilivyokuwa awali.

Idara ya nidhamu pia itahusika na kushughulikia masuala ya unyanyasaji, hii ikiwa ni kulingana na Ulrich Rhode, mtaalamu wa sheria ya Kanisa Katoliki, na kuongeza kuwa ni wazi mabadiliko hayo yanaendana na hali ilivyo sasa kufuatia msururu wa madai yaliyoligubika kanisa hilo ya unyanyasaji wa kingono.

DPAE