1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ahimiza maelewano katika ziara yake Ulaya

27 Septemba 2024

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ameonya kuhusu kuibuka kwa hali mpya ya mipasuko na uadui barani Ulaya, huku akiwatolea wito wanasiasa kuchukua hatua ya kufikiwa makubaliano kwa misingi ya uaminifu.

Luxembourg -Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis nchini Luxembourg Picha: Omar Havana/AP Photo/picture alliance

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ameonya kuhusu kuibuka kwa hali mpya ya mipasuko na uadui barani Ulaya, huku akiwatolea wito wanasiasa kuchukua hatua na kudhihirisha nia ya kufikiwa makubaliano kwa misingi ya uaminifu.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 87 ameendelea kusema kuwa migogoro mipyainaweza kuwa na matokeo ya uharibifu na kusababisha mauti huku akikumbushia kuwa vita huashiria kushindwa.

Kauli hiyo ya mkuu wa Vatican imetolewa wakati wa ziara yake nchini Luxembourg, taifa la pili kwa udogo ndani ya Umoja wa Ulaya na lenye wakazi karibu 650,000 huku asilimia 40 wakiwa ni waumini wa Kikristo. Baadaye, Papa Francis alielekea nchini Ubelgiji ambapo atakaa huko hadi siku ya Jumapili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW