1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ahimiza maelewano ya kidini Mongolia

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa mwito wa maelewano katika mkutano wa imani tofauti za kidini wakati wa ziara yake nchini Mongolia.

MongoliaI Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis na rais wa Mongolia Ukhnaagin KhurelsukhPicha: Andrew Medichini/AP/picture alliance

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa mwito wa maelewano katika mkutano wa imani tofauti za kidini wakati wa ziara yake nchini Mongolia.

Papa Francis amesema dini ndio haswa ina dhima ya kuleta maelewano katika ulimwengu uliosambaratishwa na migogoro na mafarakano. Kiongozi huyo alihudhuria mkutano uliowakutanisha wawakilishi kutoka dini tofauti nje kidogo ya mji mkuu wa Mongolia wa  Ulaanbaatar. 

Papa Francis aionya Mongolia kuhusu rushwa na uharibifu wa mazingira

Francis aliwasili Mongolia siku ya Ijumaa, akifanya ziara yake ya kwanza ya kipapa katika taifa hilo la Asia lililo katikati mwa mataifa mawili makubwa ya Urusi na China. Kiongozi huyo anatarajiwa kufanya misa mchana wa leo itakayohudhuriwa na watu wapatao elfu 2,000 mjini Ulaanbaatar.

Sambamba na Wakatoliki wa Mongolia, mahujaji kutoka China watashiriki misa ya leo. Papa Francis atasalia nchini humo hadi kesho Jumatatu kabla ya kurejea Vatican.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW