1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ahitimisha ziara yake ya Asia-Pasifiki

13 Septemba 2024

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis, amehitimisha ziara yake ya nchi za Asia Pasifiki. Papa alizuru nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu ulimwenguni, Indonesia iliyo na waumini milioni 242.

Papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis Picha: Dita Alangkara/AP/dpa/picture alliance

Ziara hiyo kwenye nchi nne za eneo hilo kuanzia Septemba Pili hadi leo, ndiyo ilikuwa ndefu na yenye changamoto zaidi kwa Papa mwenye umri wa miaka 87, ikiwa ni umbali wa zaidi kilomita 32,000

Papa Francis awasili Singapore na kulakiwa na maelfu

Wakati wa ziara hiyo, alizuru nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu ulimwenguni, Indonesia ikiwa na waumini takriban milioni 242 wa Kiislamu. Aidha alitembelea Timor Mashariki, nchi yenye idadi kubwa zaidi ya waumini wa Kikatoliki duniani baada ya Vatican.

Papa Francis alitumia ziara yake kuangazia baadhi ya vipaumbele vyake vya msingi kama Papa, ikiwemo msisitizo juu ya mazungumzo baina ya dini na tamaduni mbalimbali, kutunza mazingira na kuhimiza mambo ya kiroho kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW