1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis akamilisha ziara yake nchini Ubelgiji

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Ubelgiji leo Jumapili, kwa kuongoza misa kwenye uwanja wa Mfalme Baudouin mjini Brussles.

Brussels,  Ubelgiji | Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis Picha: &

Misa hiyo imehudhuriwa na waumini wapatao 40,000 kutoka Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa na Uholanzi.

Mchana huu papa anaondoka nchini humo na kurejea Vatikan kufuatia hafla fupi ya maagano kwenye uwanja wa ndege. Mwanzoni mwa misa hiyo, Papa alimtangaza Anne wa Yesu kuwa mtakatifu. 

Soma pia:Papa Francis amesema kashfa za unyanyaji watoto kingono ni fedheha kwa kanisa

Mwanamke huyo mwenye asili ya Hispania alikufa huko Brussels mnamo 1621 na alihusika kuanzisha nyumba za watawa katika maeneo kadhaa ikiwemo Antwerp na Tournai. 

Mwanamke huyo ambae pia alikuwa mwalimu wa kanisa Katoliki anachukuliwa kuwa moja ya wanawake maarufu katika taasisi hiyo ya kidini ulimwenguni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW