1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Papa Francis alaani Iran kuwanyonga waandamanaji

9 Januari 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kwa mara ya kwanza leo amelaani hatua ya Iran kuwauwa waandamanaji.Papa Francis pia amevitaja vita vya Ukraine kama "uhalifu dhidi ya Mungu na ubinadamu."

Bahrain | Rückreise Papst Franziskus
Picha: Maurizio Brambatti/AP Photo/picture alliance

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kwa mara ya kwanza leo amelaani hatua ya Iran kuwauwa waandamanaji. Akizungumza katika hotuba yake ya kitamaduni ya Mwaka Mpya kwa wanadiplomasia, Papa Francis pia amevitaja vita vya Ukraine kama "uhalifu dhidi ya Mungu na ubinadamu." Papa amegusia mizozo yote inayoendelea duniani ikiwemo ile iliyoko barani Afrika, Mashariki ya Kati na Asia ila kuvunja kimya chake kuhusiana na machafuko yanayoendelea Iran kufuatia kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Mahsa Amini alipokuwa mikononi mwa polisi, ndicho kikubwa kilichojitokeza katika hotuba hiyo. Waandamanaji 4 tayari wameshauwawa huku wengine wakiwa tayari wameshapewa hukumu ya kifo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW