1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis: Kashfa za unyanyasaji ni fedheha kwa kanisa

27 Septemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anayeitembelea Ubelgiji amesema kanisa hilo ni lazima "liombe msamaha" kwa "balaa" la vitendo vya unyanyasaji watoto kingono.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis Picha: ALBERTO PIZZOLI/AFP

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francisanayeitembelea Ubelgiji amesema kanisa hilo ni lazima "liombe msamaha" kwa "balaa" la vitendo vya unyanyasaji watoto kingono ambalo limeitia doa taswira ya taasisi hiyo ya kidini kote ulimwenguni.

Kwenye hotuba yake mbele ya viongozi wa kisiasa na asasi za kiraia mjini Brussells iliyofungua ziara yake ya siku tangu nchini Ubelgiji, Papa Francis amesema "visa vya unyanyasaji watoto kingono" vimelipaka tope Kanisa Katoliki na kulifedhehesha mbele ya walimwengu.

Amesema matendo hayo ni ya aibu na kanisa ni lazima litafute msamaha na kutubia. Akiwa kwenye ziara hiyo Baba Mtakatifu Francis anatarajiwa kukutana na waathirika wa vitendo vya unyanyasaji wa kingono uliofanywa na makasisi. Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo, amemtaka Papa Francis kuchukua hatua madhubuti akisema "maneno matupu hayatoshi"

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW