1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis aiombea Haiti

10 Machi 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ameliombea taifa la Haiti ambako magenge ya wahalifu yameibua machafuko katika siku za karibuni.

Haiti inakabiliwa na mzozo wa kibinaadamu kutokana na kuongezeka kwa machafuko
Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ametoa wito wa amani na maridhiano katika taifa la HaitiPicha: Alessandra Tarantino/AP/dpa/picture alliance

Papa Francis amesema anafuatilia kwa wasiwasi na maumivu makubwa mzozo unaoliathiri taifa hilo la kisiwa pamoja na mawimbi ya machafuko yanayotokea hivi karibuni huko Haiti.

Ameombea kumalizika kwa machafuko hayo na kutoa wito kwa pande zote kushirikiana ili kupata amani na maridhiano, wakati kukiwa na mwitikio mpya wa msaada wa jamii ya kimataifa.

Magenge hayo yanayodhibiti eneo kubwa la mji mkuu wa Port-au-Prince pamoja na barabara zinazoelekea kwenye maeneo mengine ya nchi yameanzisha mapambano yakijaribu kumuondoa Waziri Mkuu Ariel Henry anayeungwa mkono na nchi za magharibi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW