1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis aongoza sala maalum Kinshasa

1 Februari 2023

Siku moja baada ya kuwasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis anaongoza ibada ya hadhara leo.

Vatikan Papst-Reise in die Demokratische Republik Kongo
Picha: Arsene MPIANA/AFP

Zaidi ya waumini milioni moja wanahudhuria ibada hiyo katika uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Kinshasa. 

Baada ya ibada hiyo, Papa Francis atakutana na waathiriwa wa machafuko yanayofanyika mashariki mwa Kongo.

Waathiriwa hao walisafirishwa hadi Kinshasa kwa kuwa ziara ya Papa mashariki mwa nchi hiyo ilifutwa kwa sababu za kiusalama.

Hapo jana, Papa Francis aliyataka mataifa ya kigeni kuacha kupora rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pamoja na kulinyonya bara la Afrika. 

Soma zaidi: Papa Francis awasili Kongo, akianza ziara ya siku sita

Alipozungumza jana na viongozi wa serikali, wanasiasa, wanadiplomasia, na wawakilishi wa vyama vya kiraia baada ya kuwasili mjini Kinshasa, Papa Francis alisema ni jambo la kusikitisha kwamba Afrika inaendelea kuvumilia aina mbalimbali za unyonyaji wa kisiasa ambao umetoa nafasi kwa kile alichokiita 'ukoloni wa kiuchumi' ulio sawa na utumwa. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW