Papa Francis apanga kuzuru DR Congo na Sudan Kusini
3 Machi 2022Msemaji wa makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican Matteo Bruni amesema kuwa Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 85 ataitembelea Congo kuanzia Julai 2 hadi 7, kwa kuzuru mji mkuu Kinshasa na Goma katika mkoa wa mashariki wa Kivu Kaskazini.
Kisha atakuwa Sudan Kusini kuanzia Julai 5 hadi 7 ambapo atakuwa Juba.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako karibu asilimia 40 ya raia wakazi milioni 90 ni Wakatoliki, inakabiliana na uasi wa makundi kadhaa ya wapiganaji mashariki mwa nchi hiyo.
Ziara ya mwisho kufanywa na Papa mjini Kinshasa ilikuwa Agosti 1985, wakati John Paul II alikuwa nchini humo kwa siku mbili.
Papa Francis amefanya safari tano barani Afrika tangu alipochaguliwa 2013.
Alikuwa Kenya, Uganda ma Jamhuri ya Afrika ya Kati 2015, Misri 2017 na miaka miwili baadaye akaenda Morocco na kisha ziara ya wiki moja iliyomfikisha Msumbiji, Madagascar na Mauritius.
Chanzo: reuters