1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa Francis arejea Vatican baada ya kufanyiwa vipimo

25 Novemba 2023

Haya yanajiri wiki moja kabla ya safari ya Papa Francis kuelekea Dubai ambapo atashiriki Desemba 2 mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya Hewa wa COP28.

Papa Francis kaahirisha mikutano yake yote iliyokuwa imepangwa leo kutokana na ugonjwa wa mafua
Papa Francis kaahirisha mikutano yake yote iliyokuwa imepangwa leo kutokana na ugonjwa wa mafuaPicha: Riccardo De Luca/UPDATE IMAGES PRESS/MAXPPP/dpa/picture alliance

Uongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican umetangaza kuwa kiongozi wake Papa Francis amefanyiwa vipimo vya mapafu leo hii na hakukutwa na ugonjwa wowote. Hayo ni baada ya Papa Francis kuahirisha mikutano yake yote iliyokuwa imepangwa leo kutokana na ugonjwa wa mafua.

Haya yanajiri wiki moja kabla ya safari ya Papa Francis kuelekea Dubai ambapo atashiriki Desemba 2 mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya Hewa wa COP28, ambako anatarajiwa kukemea ukosefu wa hatua na kuhimiza kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira.

Afya ya Papa Francis imekuwa ikidhoofika katika miezi ya hivi karibuni, na kumlazimu kutumia kiti cha magurudumu na hivyo kuzusha uvumi wa kujiuzulu kwake, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Papa Benedict wa XVI.