Papa arekebisha sheria ya unyanyasaji wa kingono
25 Machi 2023Papa Francis ameitanua sheria hiyo ili kuwashirikisha pia viongozi walei wa Kikatoliki na kusisitiza kwamba watu wazima pia wanaweza kuwa waathiriwa wa unyanyasaji.
Sheria mpya zinasisitiza kuwa hata watu wazima wanaweza kuwa waathirika wa vitendo vilivyofanywa na makasisi kama vile watawa au wanaseminari ambao wanawategemea maaskofu au wakubwa wao. Awali kanisa liliwazingatia tu watu wazima wenye matatizo ya akili kama wahanga sambamba na watoto.
Sheria mpya zitawachunguza maaskofu wanaotuhumiwa kwa unyanyasaji au kuficha maovu. Aidha, inawapa mamlaka wafanyakazi wote wa kanisa kuripoti kanisani madai ya unyanyasaji ya makasisi, ingawa haiwapi mamlaka ya kuripoti polisi. Pia inawahakikishia ulinzi wanaotoa taarifa za unyanyasaji.
Chanzo: APTN