1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa Francis aruhusiwa kutoka hospitali baada ya upasuaji

16 Juni 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameruhusiwa kuondoka hospitali leo mjini Roma alikokuwa amelazwa na kufanyiwa upasuaji.

Papa Francis akiwapungia watu baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini huko Rome, Italia.
Picha: Vatican Media/REUTERS

Papa Francis mwenye umri wa miaka 86, ameondoka hospitali akiwa kwenye kiti cha magurudumu akitabasamu na kupungia mkono kundi la watu waliokuwa wamekusanyika nje ya hospitali hiyo kumtakia heri njema.

Soma Zaidi:Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, aendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Badala ya kwenda moja kwa moja Vatican, Baba Matakatifu alisimama na kusali kwa dakika kumi mbele ya sanamu ya Bikira Maria katika kanisa kuu la mtakatifu Maria, sehemu ambayo husimama mara kwa mara baada ya ziara zake nje ya nchi kwa ajili ya kutoa shukrani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW