1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Papa Francis asema vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

14 Januari 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati aliporudia wito juu ya kuleta amani nchini Ukraine na katika Mashariki ya Kati.

Papa Francis amesema vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu
Papa Francis amesema vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

 Papa Francis alisema wakati wa misa ya kila wiki kwamba binadamu wanahitaji amani na dunia inahitaji amani.

Katika maombi yake amewataka watu kutowasahau wale wanaoteseka kutokana na ukatili wa vita katika sehemu kadhaa za dunia.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mara kwa mara amekuwa anatoa wito wa kuleta amani nchini Ukraine na katika Mashariki ya Kati.

Papa Francis amesema inapasa kuwaombea wenye mamlaka juu ya migogoro ya dunia, ili watafakari juu ya ukweli kwamba vita sio njia ya kutatua migogoro, bali vinasababisha vifo kwa binadamu na madhara katika miji na miundombinu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW