1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis asikitishwa na ajali ya treni India

3 Juni 2023

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema amesikitishwa na ajali ya treni iliyotokea nchini India iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 288 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 900.

Papst Franziskus Portrait
Picha: Evandro Inetti/Zuma/picture alliance

Papa alitoa salamu zake za rambirambi pamoja na maombi kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao. 

Kadinali Mkuu wa Vatican Pietro Parolin, amesema kupitia Telegram kwamba Papa Franci pia amewaombea wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo na kuziombea pia juhudi za waokoaji za kuwatafuta manusura na miili zaidi.

Hakuna manusura wengine wa ajali ya treni India

Ajali hiyo ilitokea wakati treni ya abiria ilipoacha reli na kugongana na treni ya mizigo katika jimbo la Odisha nchini India. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW