1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ataka mapigano yasitishwe Mashariki ya Kati

13 Oktoba 2024

Wakati wa ibada ya Jumapili, Papa Francis ametoa wito wa kusitisha vita huko Mashariki ya Kati.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa FrancisPicha: Andrew Medichini/AP/picture alliance

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ametoa pia wito wa kuwaheshimu walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon ambao wamelishutumu jeshi la Israel kwa kuwashambulia kwa makusudi.

Ninaendelea kufuatilia kwa wasiwasi kile kinachotokea Mashariki ya Kati na ninatoa wito kwa mara nyingine tena na kwa pande zote kusitisha vita mara moja. Tuendeleze harakati za kidiplomasia na mazungumzo ili kufikia amani. Niko karibu na watu wote wanaohusika, iwe Palestina, Israel na Lebanon, huku nikiomba pia walinda amani wa Umoja wa Mataifa waheshimiwe, alisema Papa Francis.

Soma pia: Papa Francis asema vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

Wiki hii takriban askari watano wa kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) wamejeruhiwa na jeshi la Israel ambalo linaendelea kupambana na wanamgambo wa Hezbollah. Israel imeamuru vikosi hivyo kuhamishwa na kuondolewa katika eneo la kusini. Hadi sasa juhudi za kusaka makubaliano ya kusitisha mapigano huko Lebanon na Gaza hazijafaulu.