1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis atoa wito wa maridhiano Korea

14 Agosti 2014

Papa Francis amewasili Korea ya kusini. Papa Francis anajaribu kuzishawishi nchi hizo kuingia katika majadiliano kwa sababu utanuaji wa misuli kijeshi umechukua nafasi ya majadiliano katika mataifa hayo ya Korea.

Papst Franziskus in Südkorea 14.08.2014
Papa Francis akiwasili nchini Korea kusiniPicha: Reuters

Papa Francis anatoa wito wa kujenga utamaduni wa maelewano katika hali hii ya mivutano na wasi wasi.

"Kiu ya kupata amani katika Korea imo katika mioyo yetu, kwa kuwa italeta uthabiti katika eneo lote , itatuletea faraja kutokana na dunia kuchoshwa na vita."

Ameyasema hayo papa Francis katika ikulu ya rais nchini Korea kusini , katika kile kinachojulikana kama "nyumba ya buluu" mjini Seoul. Nae rais wa Korea kusini Park ameweza kuhisi yale aliyozungumza papa. Chini ya utawala wake ameweza kuimarisha mipaka kati ya Korea kaskazini na kusini.

Papa Francis akiingia ikulu ya Korea kusini mjini SeoulPicha: Reuters

Mataifa hasimu

Korea kaskazini na kusini ni mataifa hasimu , na lengo la kuziunganisha tena nchi hizo kama Ujerumani mbili zilivyoungana linaonekana kuwa mbali mno. Wakorea kusini wengi wanamtarajia papa atatoa ishara ya wazi.

Lakini hata kabla papa Francis kutua katika ardhi ya Korea kusini , nchi jirani ya Korea kaskazini ilitoa salaam maalum za kumkaribisha. Nusu saa kabla ya kuwasili kwa papa , Korea kaskazini ilifyatua makombora matatu ya masafa mafupi baharini, imeeleza wizara ya ulinzi ya Korea kusini. Makombora mengine mawili zaidi yalifuatia muda mfupi baadaye.

Mmoja kati ya wananchi waliokuwa wakisubiri kwa hamu kumuona papa, amesema , "nimesikia kwamba papa ni mtu mzuri sana, na watu wengi sana watakuja kumuona. Ninamatumaini kwamba papa atatoa ujumbe wa wazi kuelekea upande wa Korea kaskazini kwa ajili ya kuungana tena nchi zetu, ameongeza mtu mwingine aliyeulizwa.

Watu wakimpungia Papa Francis alipowasili Korea kusiniPicha: Getty Images

Kanisa linaamini uwezekano wa muungano

Kanisa Katoliki nchini Korea kusini linaonekana kuwa ni taasisi pekee nchini humo , ambayo bado inaamini kuhusu kuungana tena kwa nchi hizo. Mbali ya enzi za mahusiano yaliyo baridi katika mataifa hayo kanisa hilo linajaribu kupitia utoaji wa misaada ya kiutu kutositisha kabisa mahusiano.

Mara kwa mara hatua hizo zikienda kinyume na msimamo wa upinzani wa serikali ya Korea kusini. Papa Francis anaona mjadala kuwa ndio njia pekee ya kujitoa kutoka katika hali hiyo ya mkwamo.

"Ni changamoto kubwa , kuweza kuvunja kuta za kutoaminiana na chuki na kujenga utamaduni wa maridhiano na umoja. Diplomasia kama mbinu ya kuleta hali ya utulivu wa kudumu na fursa nyingi za ushawishi kwamba amani kupitia kusikilizana pamoja na midahalo ni bora kuliko kutupiana lawama, ukosoaji usio na manufaa na kuoneshana mabavu."

Papa Francis akipokewa Korea kusiniPicha: Reuters

Ziara hii ya papa katika sehemu ya Korea ni ya kisiasa. Ziara hiyo ni ya kihistoria hata hivyo , ambapo kwa mara ya kwanza ataruka juu ya ardhi ya China. Kutokana na fursa hii papa Francis ametuma simu ya maandishi kwa rais wa China Xi Jingping akiwatakia wananchi wote wa China amani na maisha bora. Ikiwa ni ishara muhimu , ambayo pia inaanzisha enzi mpya baina ya kanisa hilo na Jamhuri ya watu wa China.

Mwandishi : Tilmann Kleinjung / ZR / Sekione Kitojo.

Mhariri: Iddi Ssessanga