1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis atoa wito wa upatikanaji amani Niger

20 Agosti 2023

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameelezea matumaini yake ya kupatikana suluhu ya amani katika mgogoro wa Niger kufuatia mapinduzi yaliyofanyika katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Rom | Angelusgebet auf dem Petersplatz
Picha: Vatican Media/ANSA/ZUMA Press/picture alliance

Papa aliwaambia waumini katika uwanja wa St Peters kwamba anafuatilia matukio hayo kwa wasiwasi akiunga mkono ombi la kuwa na amani nchini humo na udhabiti katika kanda nzima ya Sahel.

Ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kupata suluhusu ya amani haraka iwezekanavyo katika mzozo huo kwa manufaa ya wananchi wa Niger. 

Abdourahamane Tchiani apanga kuwa na serikali ya mpito kwa miaka mitatu Niger

Mwezi uliopita, Kiongozi wa utawala wa kijeshi Abdourahamane Tchiani, alimpindua rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum. Bazoum, mkewe na mtoto wake wa kiume wamewekwa katika kifungo cha nyumbani katika mji mkuu Niamey.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW