1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis atuma pole kwa wahanga wa shambulizi Kongo

17 Januari 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametuma salamu za rambirambi kwa wahanga wa shambulizi la bomu kwenye kanisa la Pentekosti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Vatikan Papst Franziskus Neujahrsmesse
Picha: Andrew Medichini/AP Photo/picture alliance

Mamlaka za Kongo zimesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo la Jumapili katika mji wa Kasindi, na wengine sitini walijeruhiwa.

Soma pia: Waasi wa ADF wadaiwa kuwaua raia

Katika ujumbe wake Papa Francis ameelezea huruma na mshikamano kwa familia zote zilizoathiriwa na kuhimiza amani. Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki anatarajiwa kuwasili mjini Kinshasa tarehe 31 mwezi huu wa Januari kwa ziara ya siku tatu, ambayo awali ilijumuisha mji wa mashariki wa Goma, lakini mji huo ukaondolewa kwenye ratiba yake baada ya kuzorota kwa hali ya usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW