1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis aufungua mkutano wa kilele wa Kanisa Katoliki

2 Oktoba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ameufungua mkutano wa kilele wa viongozi wa kanisa hilo.

Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.
Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.Picha: Andrew Medichini/AP/picture alliance

Kwenye ibada ya kuufungua mkutano huo unaotambulika kama Sinodi ya Maaskofu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Papa amewaambia mamia ya makadinali, maaskofu na waumini wa kawaida wanaoshiriki kuzingatia masuala muhimu kwa ajili ya kanisa na si ya kibinafsi. 

Soma zaidi: Wakristo duniani waanza ibada ya "Kwaresma”

Mkutano huo unasogeza mbele hatua dhidi ya masuala yanayozua mgawanyiko kama la wanawake kuwa mashemasi ifikapo mwaka 2025 na kubariki ndoa za jinsia moja.

Mkutano huu wa kilele unalenga kuangazia mustakabali wa Kanisa Katoliki na unajumuisha wajumbe 368 wanaoweza kupiga kura kutoka mataifa zaidi ya 110.