Papa Francis awanyooshea mkono wapenzi wa jinsia moja
7 Agosti 2023Matangazo
Papa Francis ameyasema hayo akiwa kwenye ndege akirejea mjini Roma kutoka Ureno aliposhiriki kwenye kongamano la Siku ya Vijana wa Kikatoliki.
Alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wa habari kumuhoji kuhusu baadhi ya watu ambao ni mashoga pamoja na wanawake wasioweza kuwa mapadre kwa kushiriki huduma ya sakramenti.
Soma zaidi: Papa aruhusu mjadala wa wanawake mashemasi
Ingawa Kanisa Katoliki haliruhusu ndoa za jinsia moja, lakini Papa Francis anaunga mkono sheria inayowapa haki wapenzi wa jinsia moja katika masuala kama vile pensheni, bima ya afya na mirathi.
Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 86, alionekana katika hali nzuri kiafya na amesema kwa sasa hali yake inaimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo mwezi Juni.