Papa Francis awasili kisiwa cha Corsica nchini Ufaransa
15 Desemba 2024Kwenye ziara hiyo ya kwanza ya papa katika ksiwa hicho chenye idadi kubwa ya waumini wa Katoliki, kiongozi huyo atakutana na Rais Emmanuel Macron.
Papa Francis anakwenda Ufaransa, wiki moja baada ya shughuli kubwa ya kufunguliwa tena kanisa kuu la Notre Dame mjini Paris, ambayo alitangaza kutohudhuria, hatua iliyoibua mshangao mkubwa. Kanisa hilo, liliharibiwa vibaya kwa moto, miaka mitano iliyopita.
Mbali na kuzungumza na Macron, Papa Francis ataongoza ibada itakayokutanisha maelfu ya waumini wa Katoliki, akiwa ni papa wa kwanza kuzuru kisiwa hicho cha Corsica chenye idadi kubwa ya waumini kanisa hilo, miongoni mwa wakazi 350,000.
Hii itakuwa ziara yake ya mwisho ya nje ya nchi, kabla ya kurejea Rome kwa ajili ya msimu wenye shughuli nyingi wa Krismas.