SiasaMongolia
Papa Francis awasili Mongolia katika ziara yake ya kwanza
1 Septemba 2023Matangazo
Ziara ya Papa katika taifa hilo lenye waumini wengi wa Kibudha ni ishara ya kuunga mkono jamii ndogo ya Wakatoliki wapatao 1,400. Ametuma ujumbe wa amani na mshikamano kwa taifa jirani la China ili kukuza mahusiano.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye ndege, Papa Francis amesema:
"Kwenda Mongolia kunamaanisha kutembelea idadi ndogo ya watu katika nchi kubwa. Mongolia inaonekana kutokuwa na kikomo na ina wakaazi wachache lakini yenye utamaduni mkubwa".
Ziara ya Francis pia ni mkakati wa kuimarisha uhusiano wa Vatican na nchi jirani na Mongolia yaani China na Urusi. China haina uhusiano rasmi na Vatican.