1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis azungumzia "ukatili" unaotendeka Gaza

21 Desemba 2024

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis leo ameelezea masikitiko yake makubwa juu ya athari za mzozo wa Gaza na mashambulizi ya makombora yanayowalenga watoto kwenye ukanda huo.

Papa Francis
Papa Francis.Picha: Andrew Medichini/AP/picture alliance

Kwenye hotuba yake aliyotoa katika makao makuu ya kanisa katoliki duniani mjini Vatican, kiongozi huyo wa kiroho amesema kile kinachoendelea Gaza ni "ukatili na siyo vita", akizungumzia mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya Israel kwenye ukanda huo wa Wapalestina.

Baba Mtakatifu Francis pia amezungumzia jinsi mashambulizi hayo yalivyomzuia mwakilishi wa ngazi ya juu wa kanisa katoliki kuutembelea Ukanda wa Gaza. Papa Francis amesema hapo jana Kadinali Pierbattista Pizzaballa alizuiwa kuigia ukanda wa Gaza tofauti na alivyoahidiwa.

Vita kwenye Ukanda wa Gaza vialianza Okotba 7 mwaka jana baada ya wapiganaji wa kundi la Hamas kuishambulia Israel na kusababisha vifo vya watu 1,200.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW