1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kuanza ziara yake nchini Mongolia

31 Agosti 2023

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatarajiwa kuanza safari ya kuelekea nchini Mongolia leo Alhamisi,ambayo itakuwa ni ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na kiongozi mkuu wa kanisa hilo.

Pope Francis leads the Angelus prayer at the Vatican
Picha: Vatican Media/Handout/REUTERS

Anatarajiwa kuondoka jioni hii na kuwasili Ijumaa asubuhi katika mji mkuu wa Mongolia,Ulaanbaatar,ambako atakutana na viongozi wa nchi hiyo,watu mashuhuri pamoja na wawakilishi wa jumuiya za kiraia. 

Soma pia:Papa Francis atoa wito wa upatikanaji amani Niger

Lengo la ziara ya kiongozi huyo wa kiroho nchini Mongolia ambako Wakristo wa madhehebu ya Katoliki ni kiasi 1,500 kati ya wakaazi wake zaidi ya milioni 3,ni kuiimarisha jamii hiyo na kushajiisha  mdahalo miongoni mwa watu wa dini mbali mbali.

Ziara hiyo  ya Papa Francis mwenye umri wa miaka 86  inatarajiwa kumalizika Jumatatu wiki ijayo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW