1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kukutana na viongozi wa dini 6 huko Jakarta

Sylvia Mwehozi
5 Septemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatazamiwa leo kusisitiza utangamano wa kidini, atakapokutana na viongozi wa dini nyingine sita rasmi za Indonesia katika msikiti mkubwa zaidi Kusini-mashariki mwa Asia.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa FrancisPicha: Indonesia Papal Visit Committee

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatazamiwa hii leo kusisitiza utangamano wa kidini, atakapokutana na viongozi wa dini nyingine sita rasmi za Indonesia katika msikiti mkubwa zaidi Kusini-mashariki mwa Asia. Papa Francis anatarajiwa kutia saini tamko la pamoja na Imamu mkuu wa msikiti huo, linalohusu ulinzi wa mazingira na kudunisha utu wa binadamu unaosababishwa na migogoro, kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wa Indonesia. Papa Francis ahimiza masikizano na kuishi kwa kuvumiliana nchini Indonesia

Aidha kiongozi huyo pia ataendesha misa itakayohudhuriwa na maelfu ya watu katika uwanja wa mpira wa miguu katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta. Matukio hayo ni sehemu ya mwisho ya ziara ya siku tatu ya Papa Francis nchini Indonesia, taifa lenye idadi kubwa ya Waislamu duniani. Hapo jana Papa Francis alihimiza ustahimilivu wa kidini na kuonya kuwa maslahi binafsi ndiyo yanachochea migogoro ya kimataifa. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW