1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kuondoka hospitali Jumamosi

31 Machi 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis atatoka hospitalini hapo kesho Jumamosi na huenda akashiriki sherehe za Wiki Takatifu kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka

Italien Papst Franziskus im Krankenhaus
Picha: VINCENZO PINTO/AFP

Haya yamesemwa leo na Kadinali mmoja mkuu. Awali taarifa zilisema kwamba Papa amekuwa na usiku wa pili mtulivu hospitalini akipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu aina ya mkamba.

Soma pia: Vatican: Papa Francis amekuwa na usiku tulivu hospitalini licha ya maambukizi

Vatican inasema kwa sasa kiongozi huyo wa dini anaweza kula, kusali na kufanya kazi katika chumba chake maalum cha matibabu kilichoko ghorofa ya kumi ya hospitali ya Gemelli mjini Roma.

Awali ilikuwa imesemekana kwamba papa Francis alipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi baada ya kulalamikia matatizo ya kupumua ila baadae wahudumu katika hospitali hiyo walisema alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo wa mkamba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW