1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kuongoza ibada ya mazishi ya papa Benedict XVI

5 Januari 2023

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Fransis leo anaongoza misa ya ibada ya mazishi ya mtangulizi wake Benedict XVI mjini Vatican.

BG - Beisetzung Papst Benedikt
Picha: GUGLIELMO MANGIAPANE/REUTERS

Papa Francis atatoa mahubiri katika Misa itakayohudhuriwa na makadinali 120, maaskofu 400 na karibu makasisi 4,000 katika uwanja mkubwa wa Kanisa la Mtakafitu Petro kabla ya mwili wa Benidict wa XVI kuzikwa katika makaburi ya mapapa chini ya kanisa hilo.

Zaidi ya watu 60,000 wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo wajumbe rasmi kutoka Italia na nchini Ujerumani alikozaliwa Benedict, Mfalme na Malkia wa Ubelgiji na wakuu wa nchi au serikali wapatao 13, huku nchi nyengine zikiwakilishwa na mabalozi wao mjini Vatican.

Benedict, ambaye jina la kuzaliwa ni Joseph Ratzinger, alifariki dunia Jumamosi iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW