Papa Francis kutangaza makadinali wapya 21
9 Julai 2023Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema hii leo kwamba atatangaza Makadinali wapya 21 kutoka maeneo tofauti ya ulimwengu mwishoni mwa mwezi Septemba. Baraza hilo la Makadinali ni la tisa kuundwa chini ya Papa Francis ambaye utawala wake umefikisha miaka 10.
Uteuzi wa Makadinali wapya utakuwa ukitizamwa kwa ukaribu kama ishara ya mwelekeo wa baadaye wa Kanisa Katoliki na vipaumbele vyake kwa waumini wake wapatao bilioni 1.3.
Makadinali walio chini ya umri wa miaka 80 watashiriki katika zoezi la kumteua mrithi wa Francis. Tangu alipokuwa Papa, Francis amejaribu kuwapandisha madaraja makasisi kutoka mataifa yanayoendelea mbali na Roma kama sehemu ya falsafa yake ya ujumuishwaji.Mjadala Vatican juu ya mageuzi ndani ya kanisa Katoliki
Makadinali watakaotangazwa mwishoni mwa Septemba ni kutoka katika maeneo ambayo Ukristo unazidi kukua ikiwemo Afrika, Amerika ya Kusini na Asia.