1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ziarani kwa wanaovumiliana Mauritius

Oumilkheir Hamidou
9 Septemba 2019

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis amewasili Mauritius ambako anarajia kusherehekea, faida ya kuishi pamoja watu wa imani tofauti za kidini, na hali ya kuvumiliana ..

Vatikan | Papst Franziskus beim Angelus-Gebet
Picha: AFP/Getty Images/T. Fabi

 

Maelfu ya waumini wamekusanyika katika mji mkuu Port-Louis, baadhi yao kabla ya alfajiri kuingia, wakimsubiri kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwengu mwenye asili ya Argentina kuhutubia katika kisiwa hicho kidogo cha bahari ya Hindi.

Papa Francis ataongoza misa katika jengo la amani la Mary Queen , jenego lile lile la milimani ambako Johanna Paulo wa pili alihutubia alipofika ziarani kwa mara ya mwisho Mauritius mwaka 1989.

"Zaidi ya waumini 3500 miongoni mwetu wametokea Reunion, kisiwa kilichoko umbali wa kilomita 175 kutoka Mauritius, anasema Josette ambae ni miongoni mwa waliokuwa wakimsusbiri Papa Francis.

"Ni muhimu kwetu sisi kukutana na Papa, ni fursa ya aina pekee, amesema kwa upande wake Genevieve, raia wa Mauritius mwenye umri wa miaka 47. Visiwa vya Mauritius vina jumla ya wakaazi milioni moja na laki tatu, wengi wao ni wa madhehebu ya Hindu. Kuna jamaii za wachache za wakristo na waislam pia. Mauritius iliyowahi kutawaliwa na wadachi, wafaransa na waingereza kabla ya kujipatia uhuru mwaka 1968, imeibuka toka nchi masikini na kugeuka kuwa miongoni mwa nchi tajiri za Afrika.

Mauritius,mfano mzuri wa kuishi pamoja kwa amani jamii za waumini tofauti

Mauritius ni kituo cha mwisho cha ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni iliyomfikisha kabla ya hapo kisiwani Madagascar na Msumbiji.

Waziri mkuu wa Mauritius  Pravind Kumar Jugnauth amesema Papa "atajionea mfumo wa kweli wa kuishi pamoja watu wa jamii mbali mbali"."Mchanganyiko wa tamaduni zetu haujawahi kuwa pingamizi kwetu katika kuimarisha mazungumzo, hali ya kuelewana na amani" amesema. Kwa upande wake Askofu mkuu wa Port Louis, kardinal Maurice Piat amesema kabla ya Papa kuwasili visiwani humo tunanukuu:"hii si ziara ya Papa kwa wakristo peke yao, bali pia kwa wa Mauritius wote na kwa mchanganyiko wa jamii zake zote"-mwisho wa kumnukuu askofu mkuu wa mji mkuu wa Mauritius , Port Louis.

Ziara ya Papa Francis inatokea wakati wa kuandhimisha amiaka 155 tangu alipofariki dunia padri Jacques Desire Laval, aliyefariki dunia mwaka 1864 na kutangazwa mwenye heri mwaka 1979.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri: Zainab Aziz

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW