1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Papa: Kanisa nchini Papua New Guinea liwasaidie wanawake

7 Septemba 2024

Papa Francis aliye ziarani nchini Papua New Guinea amelitolea mwito kanisa kwenye taifa hilo la kanda ya Pasifiki kuwaweka karibu wanawake waliotengwa na jamii au kufanyiwa vitendo vya kikatili.

Papa Francis
Papa Francis. Picha: Tiziana Fabi/AFP/Getty Images

Papa Francis ametoa rai hiyo baada ya kusikiliza simulizi za madhila wanayopitia wanawake kwenye nchi hiyo ambako ukatili dhidi yao unatajwa kuwa zaidi ya mara mbili ya kiwango cha maeneo mengine duniani.

Wengi hushambuliwa au kutuhumiwa kwa uchawi na ushirikina na kisha familia zao huwatenga au kuwatelekeza. Baba Mtakatifu Francis amesema ni wajibu wa kanisa kuwaweka karibu waathiriwa wa vitendo vya aina hiyo kwa kuwaonesha upendo na kufanyia wema.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa asilimia 60 ya wanawake nchini Papua New Guinea hupitia aina fulani ya unyanyasaji wa kimwili au kingono kutoka kwa wenza wao.