1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa akutana na wahanga wa unyanyasaji wa kingono

20 Oktoba 2025

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV, amekutana kwa mara ya kwanza na kundi la wahanga wa unyanyasahi wa kingono unaodaiwa kufanywa na makasisi wa kanisa hilo.

Vatikan 2025 | Papa Leo XIV
Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Leo XIV.Picha: Filippo Monteforte/AFP

Tim Law, muanzilishi mwenza wa taasisi ya Ending Clergy Abuse (ECA), iliyoko Marekani  iliyo na lengo la kusitisha unyanyasaji unaodaiwa kufanywa na makasisi amesema, nia hasa ya mkutano huo ni kuwa na uhusiano mwema na Papa Leo  na kupata hakikisho lake la kujadili masuala haya kwa uwazi. Amesema Papa ameridhia matakwa yao.

Tim ameongeza kuwa mkutano huo uliowahusisha pia mawakili wanaowawakilisha wahanga haokutoka zaidi ya mataifa 30 ulipaswa kufanyika kwa dakika 20 tu lakini ulirefushwa hadi saa moja. 

Kundi hilo limemtaka Papa Leo  kuweka sheria ya kutovumilia unyanyasaji na kukomesha kabisa dhuluma hiyo. Amesema tayari sheria hiyo inafanya kazi nchini Marekani kwa makanisa yote.  makanisani.  ambayo tayari imewekwa nchini Marekani kwa 

Chini ya sheria iliyoundwa na maaskofu wa Marekani, kasisi anapaswa kuondolewa kikamilifu kutoka katika huduma za kikanisa iwapo kisa chochote cha unyanyasaji wa kingono wa watoto chini ya miaka 18 kitakachothibitishwa dhidi yake. 

Wahanga hao wamesema hayo, siku chache tu baada ya Tume ya Vatican ya kuwalinda Watoto kuwashutumu viongozi wa ngazi ya juu kanisani humo kusuasua katika suala zima la kuwasaidia wahanga.Kwa miongo mingi, kanisa Katoliki limekuwa likitikiswa na kadhia ya kuficha uovu huo, hali ambayo inachafua jina na sifa ya kanisa mbali na hasara ya mamilioni ya dola kulipa fidia.

Mwezi Mei ECA awali ilikuwa imemuandikia barua Papa Leo XIV,ikiomba kukutana na kiongozi huyo wa kiroho baada ya kuchaguliwa kama kiongozi wa  waumini takriban bilioni 1.4 duniani.

Vatican ilithibitisha Papa Leo kukutana na wajumbe wa ECA , lakini haikutoa taarifa zaidi ya kile kilichozungumzwa. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW