1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo ahimiza amani akiwa kwenye ziara yake Algeria

15 Aprili 2026

Kiongozi huyo mkuu wa kanisa katoliki duniani, amekemea vita na migogoro aliyosema imeunyong'onyeza moyo wa Mungu

Papa Leo anafanya ziara ya siku 10 barani Afrika inayozijumuisha nchi nne
Papa Leo anafanya ziara ya siku 10 barani Afrika inayozijumuisha nchi nnePicha: Gregorio Borgia/AP Photo/picture alliance

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ametembelea chimbuko lake la kiimani katika eneo la kale alikozaliwa Mtakatifu Augustine katika mji wa Annaba, nchini Algeria.

Papa Leo alivutiwa kujiunga na upadri kutokana na utumishi wa mwanatheolojia huyo aliyeacha taathira katika ulimwengu wa Ukristo.

Ameliambia kundi dogo la watawa na wazee katika mji huo wa Annaba, kwamba moyo wa Mungu umenyong'onyezwa na vita, vurugu, ukosefu wa haki na uwongo.

Papa Leo XIV kufanya ziara mjini Annaba nchini Algeria

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa kiroho wa Kanisa Katoliki duniani nchini Algeria, ambako Papa Leo analenga kusisitiza kuhusu ujumbe wa amani pamoja na mshikamano kati ya Wakristo na Waislamu, akitumia muongozo wa Mtakatifu Augustine.

Ziara hiyo ya Papa imekumbwa na mashambulizi mawili ya kujitowa muhanga yaliyotokea katika mji wa Blinda, ulioko kilomita 45 kutoka mji mkuu, Algiers. Kesho Jumatano ataanza ziara yake nchini Cameroon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW