1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo ahimiza mshikamano na matumaini mapya Lebanon

1 Desemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV alihimiza mshikamano na matumaini mapya katika Lebanon inayokabiliwa na migogoro akipongeza ‘ustahimilivu' wa nchi hiyo licha ya miaka ya migogoro na misukosuko.

Lebanon Beirut 2025 | Papa Leo wa XIV wakati wa sherehe ya makaribisho katika Uwanja wa Ndege wa Beirut.
Lebanon Beirut 2025 Papa Leo wa XIV wakati wa sherehe ya makaribisho katika Uwanja wa Ndege wa Beirut.Picha: VATICAN MEDIA/ANSA/picture alliance

Katika sehemu ya pili ya ziara yake ya kwanza ya nje, baada ya kusimama nchini Uturuki, Papa alikutana na Rais wa Lebanon Joseph Aoun na maafisa wakuu katika ikulu ya rais jijini Beirut. Kiongozi huyo alisikika akisema heri wapatanishi  wale wanaochagua amani hata pale migogoro inapokuwa rahisi. Kabla ya ziara hiyo, mabango kwenye barabara zilizokarabatiwa yalimkaribisha Leo kama ‘Papa wa Amani. Na tayari ametangaza nia yake ya ‘kutangaza tena ujumbe wa amani katika Mashariki ya Kati' na kuimarisha jumuiya za Kikristo kote katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW