Papa Leo aitaka Mashariki ya Kati iachane na ukatili wa vita
2 Desemba 2025
Matangazo
Papa Leo amewataka viongozi hao waubadilishe mwenendo wao na waachane na ukatili wa mapigano.
Papa ameyasema hayo alipouhutubia umati wa watu laki moja na nusu wakati wa misa takatifu huko mjini Beirut.
Ameusihi uongozi wa Lebanon pia kutafuta suluhu la miaka ya machafuko, migogoro ya kisiasa na uchumi uliosambaratika.
Amesema eneo zima la Mashariki ya Kati linahitaji mwongozo mpya ili kukuishinda migawanyiko ya kisiasa, kijamii na kidini.
Kiongozi huyo wa kidini amekuwa katika mkumbo wa pili wa ziara yake ya siku tatu nchini Uturuki na Lebanon.