1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo ameombea amani kwa taifa la Syria na Iran

11 Januari 2026

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV amewaombea watu wote waliouawa katika maandamano ya Iran na katika mzozo wa Syria akitoa wito wa majadiliano na amani, katika ibada yake ya kila wiki mjini Vatican.

Vatikanstadt 2026 | Papst Leo XIV
Papa Leo ameombea majadiliano na amani kwa taifa la Syria na Iran Picha: Alessandra Tarantino/AP Photo/picture alliance

Amesema fikra zake mara zote zipo eneo la Mashariki ya kati  hasa Iran na Syria, ambako mivutano iliyopo inasababisha mauaji ya watu wengi. Papa Leo ambae ni raia wa Marekani, amesema anayaombea maeneo hayo kuwa na amani kwa manufaa ya jamii kwa ujumla.

Papa anayewaongoza waumini wa kikatoliki bilioni 1.4 duniani, pia amewaombea watu wa Ukraine, kufuatia mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya taifa hilo jirani.

"Nchini Ukraine, mashambulizi mapya na makubwa zaidi, hasa yanayolenga miundombinu ya nishati, yanawaathiri pakubwa raia, huku hali ya hewa ya baridi ikizidi kuwa mbaya. Ninawaombea wale wanaoteseka na narudia wito wangu wa kukomesha vurugu na kuongezwa kwa juhudi za kufikia amani."

Juhudi za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Ukraine bado hazijafanikiwa licha ya matumaini ya kupatikana mkataba wa amani yanayotolewa kila wakati na pande hizo hasimu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW