1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo kupeleka ujumbe wa amani Uturuki na Lebanon

25 Novemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo wa XIV atafanya ziara yake ya kwanza nje ya Italia atakapoelekea Uturuki na Lebanon, anakotarajiwa kupeleka ujumbe wa amani katika eneo hilo.

Vatikanstadt Vatikan 2025 | Papst Leo XIV feiert Messe zum Jubiläum der Armen im Petersdom
Picha: Riccardo De Luca/Anadolu Agency/IMAGO

Baba Mtakatifu Leo anatarajiwa kutoa wito wa umoja miongoni mwa makanisa ya Kikristo yaliyogawika.

Kiongozi huyo wa kidini atatoa hotuba yake ya kwanza kwa mataifa ya kigeni na azuru maeneo ya kitamaduni katika ziara yake hiyo ya Novemba 27 hadi Disemba 2.

Mtangulizi wake Papa Francis alikuwa amepanga kufanya ziara katika nchi zote mbili ila hakuweza kutokana na afya yake iliyokuwa inazidi kuzorota.

Papa Francis alifariki dunia Aprili 21 na Leo akachaguliwa kuwa Baba Matakatifu mnamo Mei 8.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW