1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Papa Leo: Vita vya Mashariki ya kati ni janga la kibinaadamu

22 Machi 2026

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV amesema vifo na mateso yanayosababishwa na vita Mashariki ya Kati, ni janga kubwa la kibinaadamu duniani.

Vatikan 2026 | Papst Leo XIV
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV Picha: Alberto Pizzoli/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo wa kidini ameyasema hayo huku akiendeleza wito wake wa kutaka vita hivyo visitishwe mara moja.

Wakati vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran vikiingia wiki yake ya nne , Papa huyo wa kwanza kutoka Marekani, amesema anafuatilia kwa hofu kubwa hali ya Mashariki ya kati na maeneo mengine yanayokumbwa na vita.

"Ninaendelea kufuatilia kwa masikitiko makubwa hali ilivyo Mashariki ya Kati, na pia katika maeneo mengine ya dunia yanayokumbwa na vurugu. Hatuwezi kukaa kimya wakati watu wengi wasiokuwa na hatia, ambao ni waathirika wa vita hivi wakiumia. Kinachowaumiza kinawaumiza wanadamu wote. Vifo na mateso vinavyosababishwa na vita hivi ni janga kwa dunia nzima na hata mbele za Mungu."

Akizungumza katika uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Peter, Papa Leo, amesema ni muhimu kuomba ili kukemea uchokozi na ukatili unaoendelea duniani ili  kufungua njia ya uwepo wa amani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW