1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo wa XIV ahimiza amani duniani

14 Aprili 2026

Kiongozi huyo wa juu zaidi wa kanisa katoliki duniani anaendelea na ziara yake barani Afrika akiwa katika siku ya pili katika kituo chake cha kwanza cha ziara hiyo nchini Algeria

Papa Leo wa XIV ni kiongozi wa kwanza wa juu wa  kanisa katoliki kuitembelea Algeria
Papa Leo wa XIV ni kiongozi wa kwanza wa juu wa kanisa katoliki kuitembelea AlgeriaPicha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo wa XIV ametowa mwito wa amani na kumalizwa kwa tabia ya ukoloni mamboleo inayoendelea duniani.

Matamshi hayo ya papa aliyatowa mwanzoni mwa ziara yake nchini Algeria jana na kuandamwa na kauli za kushambuliwa vikali kwa maneno na Rais Donald Trump na makamu wake JD Vance, baada ya kukosoa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Papa Leo XIV kufanya ziara mjini Annaba nchini Algeria

Hivi leo kiongozi huyo wa kiroho anatarajiwa katika mji wa Annaba ambako atatembea kufuata nyayo za Mtakatifu Augustino, mwanatheolojia aliyekuwa na taathira kubwa katika Ukristo. Ataendesha misa katika kanisa kubwa la Mtakatifu Augustino mbele ya viongozi wa kanisa hilo kutoka barani Afrika.

Papa Leo ni kiongozi wa kwanza wa juu wa Kanisa Katoliki duniani kuitembelea Algeria, ambacho ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya mataifa manne ya Afrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW