1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV ahimiza usitishaji mapigano wakati wa Krismasi

24 Desemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ametoa wito kwa "watu wenye nia njema” kusitisha mapigano kwa saa 24 katika maeneo yote ya vita duniani wakati wa sherehe za Krisimasi.

Papa Leo ameelezea masikitiko yake baada ya ombi la kusitisha mapigano kwa alau kwa muda mfupi kukataliwa na  na Urusi, ikizingatiwa ongezeko la mashambulizi makubwa ya hivi karibuni dhidi ya Ukraine.

Kiongozi huyo wa kiroho ambaye alianza kuhudumu mwezi Mei, ataongoza Misa yake ya kwanza ya Krismasi usiku wa leo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambako anatarajiwa kulaani vita na vurugu na kukumbusha mateso ya raia.

Katika tamko lake la awali , Papa Leo alizungumzia hali ya Mashariki ya Kati, akisema wakaazi wa eneo hilo wanajaribu kusherehekea Krisimasi licha ya mazingira magumu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW