1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV alaani dunia kushindwa kumaliza njaa

16 Oktoba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mataktifu Leo XIV Alhamis ameikosoa hatua ya dunia kushindwa kuwazuia mamilioni ya watu kukabiliwa na njaa, wakilalamikia hali mbaya ya kiuchumi.

Vatikan Vatikanstadt 2025 | Papst Leo XIV. bei der Jubiläumsmesse der Marianischen Spiritualität
Picha: Alberto Pizzoli/AFP

Papa Leo ameitaka dunia kujitafakari kuhusu mitindo yao ya maisha na vipau mbele vyao.

"Kuwaruhusu mamilio ya binadamu waishi - na kufa - wahanga wa njaa ni kushindwa kwa pamoja na dhambi ya kihistoria," alisema Papa katika hotuba aliyoitoa katika shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo lililo na makao yake huko Roma.

"Janga la njaa linazidi kuikumba sehemu kubwa ya binadamu," alisema hayo siku moja bada ya Umoja wa Mataifa kutahadharisha kuwa njaa duniani imefikia viwango vya rekodi.

Wapalestina wakisubiri mgao wa chakula huko Khan YounisPicha: Doaa Albaz/Middle East Images/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo wa dini amezungumzia hali ambapo kiasi kikubwa cha chakula kinatupwa duniani wakati ambapo mamilioni ya watu wanahangaika kupata chochote cha kutia kinywani.

Amezungumzia hasa yanayoendelea "Ukraine, Gaza, haiti, Afghanistan, Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Yemen na sudan Kusini," miongoni mwa nchi nyengine ambako umaskini umekuwa jambo la kawaida.

Amelaani pia hatua ya ulimwengu kuonekana kusahau suala la njaa kutumika kama silaha ni uhalifu wa kivita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW