Papa Leo XIV atoa wito wa amani wakati wa ibada ya Pasaka
5 Aprili 2026
Matangazo
Akihubiria umati mkubwa wa waumini waliojitokeza kwa sherehe za Pasaka katika uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatican, Papa Leo amesema watu wanazidi kuzoea vurugu na kuwa na kasumba ya kutojali kuhusu vifo vya maelfu ya watu.
Kiongozi huyo wa takriban Wakatoliki bilioni 1.4 duniani, ambaye alichaguliwa Mei 2025, pia alitoa wito wa kukesha kwa maombi huko Vatican mnamo Aprili 11.
Papa Leo pia alitoa heshima kwa mtangulizi wake Papa Francis ambaye mara ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa Jumapili ya Pasaka mwaka jana saa chache kabla ya kifo chake.
Huko mjini Jerusalem, kulikuwa na ukimya katika vichochoro vya mji mkongwe, uliochochewa na mzozo wa Israeli huko Gaza na sasa vita vya Mashariki ya Kati.