1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV atoa wito wa msamaha nchini Algeria

14 Aprili 2026

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amewasili mjini Algiers, Algeria kwa ziara ya kihistoria katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi na akatoa wito wa msamaha kwa waathiriwa wa vita vya uhuru nchini humo.

Vatican City 2026 | Papa Leo XIV.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV akiongoza maombi katika kanisa la Mtakatifu Petro huko Vatican mnamo Aprili 11, 2026Picha: Isabella Bonotto/Anadolu/picture alliance

Akitoa hotuba ya heshima kwa waathiriwa wa vita vya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Ufaransa vya mwaka 1954-1962, Papa Leo alitoa wito wa "msamaha.

''Mahali hapa tukumbuke kuwa Mwenyezi Mungu anataka amani kwa kila taifa, amani ambayo si ya kukosekana kwa migogoro tu, bali ya kielelezo cha haki na utu.  Amani hii ambayo inatuwezesha kuangazia siku zijazo kwa roho ya upatanisho, inawezekana tu kupitia msamaha.''

Muda mfupi kabla ya kuondoka Roma, papa huyo mzaliwa wa Marekani alikosolewa hadharani na Trump Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alikashifu matamshi ya Papa Leo ya kutaka kusitishwa kwa vita nchini Iran.

Akiwa ndani ya ndege, Papa Leo aliwaambia waandishi wa habari kwamba

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW